loader
Dstv Habarileo  Mobile
Wanafunzi kukaa chini, JPM atuma salamu kwa viongozi Dar

Wanafunzi kukaa chini, JPM atuma salamu kwa viongozi Dar

RAIS John Magufuli ametuma salamu kwa viongozi wa Wilaya ya Ubungo kufuatia wanafunzi wa Shule ya King'ongo  iliyopo Manispaa ya Ubungo kukaa chini na kwamba wajiandae akitoka Bukoba anakuja Ubungo.

Magufuli ameyasema hayo mara baada ya kuzindua Shule ya Sekondari ya Ihungo  mjini Bukoba leo.

”Kuna shule moja ya msingi Ubungo, Dar Es Salaam inatwa King'ongo, ina wanafunzi wengi tu. Shule hiyo wanafunzi bado wana kaa chini, madarasa mengine yamebomoka, madawati mengine yamevunjika yameachwa bure.

“Mkuu wa Wilaya yupo, Mkuu wa Mkoa yupo, Mkurugenzi wa Ubungo bado anakusanya kodi yupo na Mbunge wa Ubunge yupo tena yupo hapa na ni profesa tena wa Elimu, simama profesa (Kitila Mkumbo) wakuone kwenye jimbo lako, anafundisha elimu, mimi napenda kusema uwazi,”amesema Rais Magufuli.

”Tena wanazungukia maeneo hayo, lakini hiyo shule ya Ubungo King'ongo, wanakaa chini na wanaona, nina mshukuru huyo mwandishi ameitoa kwenye mitandao, viongozi wa kule wakaanza kusema ni masuala ya kisiasa, hayo sio masuala ya kisiasa hayo ndiyo ninayopenda kuyajua.

“Ninazungumza nikiwa Kagera lakini nikienda Dar Es Salaam niyakute hayo madarasa yamekamilika na wanafunzi hawakai chini, nitaenda kuitembelea hiyo shule kama wananisikia wa Dar es Salaam ujumbe umefika.” amesema.

“|Wanafunzi kukaa chini hii ni dhambi kubwa sana kwangu,  nilikosea kuwachagua baadhi ya viongozi  na ndiyo maana nilipofika hapa nikawa navamia madarasa nikakuta madawati yapo, nikasema haleluya hongereni sana, lakini hiyo shule ya Ubungo maneno haya wayasikie, meseji sent and delivery.

“Kuna maeneo watu wanafanya kazi vizuri sana, kuna maeneo mengine bado wamelala, ndio maana Mkurugenzi wa Geita niliamua kumfukuza kazi, yeye ananunua gari la Sh Milioni 400, huku wananchi wanachangishwa kwa ajili ya kununua madawati, mimi nimemaliza, salamu ziwafikie,”asisitiza JPM

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/75fcea978e9311aa6981e882a5397e94.jpg

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, ameweka jiwe la ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi