loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Muhtasari wa hukumu kwa Kiswahili kuanzia Feb.

MAHAKAMA ya Tanzania itaanza kutoa muhtasari wa hukumu kwa lugha ya Kiswahili kuanzia Februari mwaka huu ikiwa ni sehemu ya mchakato wa kuanza kuendesha shughuli zote za Mahakama kwa lugha hiyo.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma, ameyasema  hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumzia maadhimisho ya Siku ya Sheria yanayotarajiwa kufanyika Februari Mosi, mwaka huu.

Maadhimisho hayo yatafanyika sambamba na Maadhimisho ya Miaka 100 ya Mahakama Kuu Tanzania.

Profesa Juma amesema, uendeshaji wa shughuli za Mahakama kwa lugha ya Kiswahili ni suala muhimu, lakini linahitaji umakini kulitekeleza.

"Mwishoni mwa mwaka jana, Mheshimiwa Waziri wa Sheria alitutembelea, tulizungumza kwa kina kuhusu uendeshwaji wa shughuli zote za Mahakana kwa lugha ya Kiswahili, lakini ni suala linalohitaji umakini mkubwa.

Hili suala ni muhimu sana na tayari katika Mahakama ya mwanzo shughuli zote zinafanyika katika lugha ya Kiswahili," amesema.

Profesa Juma amesema kwa sasa ni sahihi kusema Kiswahili kinatumika kwa asilimia 70 katika shughuli za kimahakama kwa sababu Mahakama hizo za mwanzo ndizo zinazosikiliza asilimia 70 ya mashauri yote.

Amesema, katika Mahakama nyingine ni kumbukumbu tu za kimahakama ndizo zinaandikwa Kiingereza, lakini shughuli nyingine zinafanyika kwa Kiswahili isipokuwa pale inapolazimu kutumia lugha ya Kiingereza.

Mtaalamu wa Lishe ya Binadamu kutoka ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi