loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

DC: Wapokeeni watoto hata bila sare

MKUU wa Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa, Said Mtanda, amewapa siku saba wanafunzi 1,641 wawe wamejiunga kidato cha kwanza kwenye shule walizopangiwa.

 

Aliagiza walimu wakuu wawapokee wanafunzi hao hata kama hawana sare za shule na wanatembea bila kuvaa viatu.

 

"Wabunge, madiwani, wataalamu, maofisa elimu kata, maofisa tarafa, watendaji wa vijiji na kata pia Ofisa Elimu Elimu ya Msingi Wilaya wahakikishe wazazi na walezi watoto wao wanaripoti shuleni kwa wakati vinginevyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao" alisema Mtanda.

 

Alitoa maelekezo hayo alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu kufunguliwa kwa shule za msingi na sekondari na wanafunzi walioripoti kidato cha kwanza wilayani humo.

 

Alisema, wanafunzi ambao hawajajiunga na kidato cha kwanza katika shule walizopangiwa wilayani humo tangu zifunguliwe Januari 11 mwaka huu ni sawa na asilimia 40 ya wanafunzi 4,301 waliochaguliwa.

 

Kuhusu miundombinu ya vyumba vya madarasa alisema, wilaya hiyo haina changamoto ya upungufu kwa kuwa mwaka uliopita ujenzi wa majengo 560 ya shule za msingi na sekondari ulikamilika.

KATIBU Mkuu Ofisi ya Rais, ...

foto
Mwandishi: Peti Siyame, Sumbawanga

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi