loader
Dstv Habarileo  Mobile
JPM: Mjipange asiyetaka aondoke

JPM: Mjipange asiyetaka aondoke

RAIS John Magufuli amewataka wasaidizi wake kujipanga kwani katika miaka yake ya uongozi iliyobakia  atakuwa mkali sana na hatokubali kukwamishwa.

Magufuli ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wananchi wa Misenyi  akiwa njiani kwenda Karagwe kuweka jiwe la msingi la kiwanda cha maziwa cha Kahama Fresh.

Magufuli alisema wasaidizi wake wakiwemo mawaziri na wakuu wa mikoa wasiotaka kufanya kazi waache kazi na na kwamba ni kipindi cha mwisho kwake na hatogombea tena.

“Wateule wangu mjipange kweli kweli, nataka yale yote niliyoyaaidi niyatekeleze katika kipindi changu cha miaka mitano, nitakapoondoka niwe nimekamilisha ahadi zangu zote, ni muhula wangu wa mwisho, sitakubali mtu anicheleweshe, atakayenichelewesha atachelewa yeye,” amesema

Aidha Magufuli amesema atausimamia mradi wa maji wa Kyaka ukamilike na akamuonya mkandarasi kuwa akishindwa kuukamilimisha ndani ya muda uliopangwa ataondoka.

“Na Naibu Waziri ukamweleze Waziri mwezako, na ninyi wabunge mkamweleze Waziri kwamba huu mradi nataka uishe. Huyu mkandarasi kama hawezi kufanya kazi fukuzeni, hakuna kubemelezana hapa, hatukuja kubembelezana, hapa ni kazi tu. Contractor (mkandarasi) usipofanya kazi vizuri unaondoka…nataka maji”alisema Rais Magufuli.

Mradi huo unahusisha ujenzi wa chanzo cha maji kwenye Mto Kagera chenye uwezo wa kuzalisha lita za maji 6,574,000 kwa siku; ulazaji wa bomba kuu kutoka kwenye chanzo hadi kwenye kituo cha tiba ya maji; ujenzi wa kituo cha tiba ya maji kitakachokuwa na tenki la kuhifadhia maji.

Kukamilika kwa mradi huo kutanufaisha wananchi wa maeneo ya Kyaka, Bunazi na maeneo mengine yanayozunguka mradi wilayani Missenyi mkoani Kagera.

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi