loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Maalim Seif ataka vyama visiwagawe Wazanzibari

MAKAMU wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalimu Seif Sharif Hamad amesema misimamo ya vyama vya siasa isitumike kusababisha mifarakano na kuwagawa wananchi wa Zanzibar.

Amesema jamii nyingi zimefarakana na kutengana kwa sababu ya misimamo ya kisiasa na amewataka wananchi wabadilike na waendane na kasi ya Serikali ya Awamu ya Nane inayoongozwa na Rais Dk Hussein Mwinyi katika kuwaunganisha wananchi.

Maalim alisema hayo jana wakati akizungumza na wananchi wa mkoa wa Kaskazini B, Bumbwini, Unguja akiwa katika ziara za kuhimiza mshikamano wa maridhiano ya kisiasa visiwani hapa.

Alisema kabla ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964, wananchi wa Zanzibar waligawanyika kutokana na misimamo ya vyama vya siasa na mara baada ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 watu waliingia katika chuki za kisiasa.

Alisema Rais wa kwanza wa Zanzibar, Sheikh Abeid Amani Karume alitunga Sheria Namba 6 ya Mwaka 1964 iliyokuwa na lengo la kuweka umoja wa Wazanzibari wote na kuondoa chuki kwa misingi ya kikabila.

‘’Hayo ndiyo malengo ya Mapinduzi ya Zanzibar kuondoa misingi ya aina zote za matabaka ikiwamo dini na rangi ili kuleta mshikamano na kufanya kazi kuleta maendeleo,’’ alisema Maali Seif.

Aliwataka wananchi kumunga mkono Rais Mwinyi ambaye ameonesha umuhimu wa kuwapo kwa maridhiano ya kisiasa kwa ajili ya kumaliza siasa za chuki na uhasama Zanzibar.

‘’Huu ni wakati wa kumuunga mkono Rais wetu Dk Mwinyi katika kufikia maridhiano ya kweli ya kuwaunganisha wananchi wa Zanzibar na kumaliza siasa za chuki na uhasama,’’ alisema Maalim Seif.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Ayoub Mohamed Mahmoud aliwataka wananchi wabadilike na wawe na malengo na mtazamo wa maridhiano ya kisiasa kwa ajili ya kuleta maendeleo.

Alisema Serikali ya Awamu ya Nane imejikita kuimarisha uchumi wa bluu na kuwawezesha wajasiriamali kupiga hatua za maendeleo.

‘’Hatuwezi kufikia maendeleo ya kweli ikiwamo uchumi wa bluu na uwekezaji kama miongoni mwetu tutakuwa tukitofautiana na kujenga chuki na uhasama,’’ alisema Mahmoud.

MKUU wa Mkoa (RC)  wa Mwanza, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Zanzibar

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi