loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

NARCO toeni maeneo kwa wafugaji

RAIS John Magufuli amepigilia msumari wa mwisho kwa kuitka Kampuni ya Ranchi ya Taifa (NARCO), kutoa maeneo ambayo hayajaendelezwa kwa wafugaji.

Rais Magufuli alisema kuna maeneo ambayo hayatumiki na ndio maana mifugo haiongezeki hivyo wapatiwe wafugaji.

“Natambua NARCO tuna maeneo mengi lakini hatuyatumii ipasavyo, nafahamu Kongwe kuna ng’ombe 800 wana mimba, lakini hawaongezeki, wafugaji wa kawaida ng’ombe wao wanaongezeka, hata wa kwangu wanaongezekana, ila nyie  hawaongezeki sasa toeni hayo maeneo kwa wafugaji,” alisema Magufuli.

Alisema wafugaji wapewe maeneo hayo kwa kukodishwa na gharama nafuu na kwamba Narco wafikirie faida  watakayoipata mbele.

Pia Rais Magufuli aliwaomba wananchi kuwekeza kwenye sekta ya mifugo na kwamba mwekezaji sio lazima atoke nje ya nchi.

Kauli ya Magufuli imekuja baada ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi,  Mashimba Ndaki  baada ya Januari 14 kutoa siku 10 zinazoisha Jumamosi ijayo Januari 23 kwa  Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) kubaini na kuwanyang’anya maeneo, wawekezaji waliopatiwa vitalu katika ranchi za taifa ambao wamebadili matumizi ya ardhi kinyume na makubaliano ya mikataba yao.

Mtaalamu wa Lishe ya Binadamu kutoka ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi