Rais Donald Trump wa Marekani ambaye leo anamaliza muda wake ametoa hotuba ya mwisho ambapo amejinadi kuwaTaifa la Marekani amelifanyia mengi ikiwa pamoja na kutoanzisha vita, kurudisha wanajeshi nyumbani na kufanya maamuzi mengi magumu yenye maslahi kwa taifa hilo.
VIDEO>>>Mambo yatakayotokea leo Biden akiapishwa kuwa Rais, Trump aingia mitini
Katika hotuba yake ya dakika 20, Trump amewashukuru wote alioshirikiana nao katika uongozi wake wa miaka minne bila kujali wakosoaji na wote waliokuwa wakipinga maendeleo ya taifa hilo.
Trump amekiri kuwa hatohudhuria hafla ya uapisho wa rais mteule Joe Biden, itakayofanyika leo huko Washington DC, Marekani.