loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

JPM: Kunyweni maziwa

RAIS John Magufuli amewataka watanzania kunywa maziwa kwa wingi kwani   hivi sasa mtu mmoja anakunywa wastani wa lita 54.7 kwa mwaka, kiwango ambacho ni kidogo.

Rais Magufuli aliyasema hayo jana wakati akiweka jiwe la msingi katika kiwanda cha Maziwa cha Kahama Fresh kinachojengwa na mwekezaji wa Ndani katika Kata ya Kihanga wilayani Karagwe

Alisema mpaka sasa kiwango cha maziwa kinachotumiwa na mwananchi ni kidogo ukilinganisha na viwango vinavyotakiwa na shirika la afya ulimwenguni (WHO).

Kwa upande wa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki alisema “Unywaji wa maziwa  ni mdogo zaidi ya malengo ya Ukanda wa Afrika ambao unatakiwa lita 74 kwa mwaka na pungufu ya viwango vya Shirika la Chakula Duniani (FAO) ya kunywa lita 200 kwa mwaka.

Alisema wazalishaji wanatakiwa kuendelea kuongezeka, kwani soko ni kubwa ndani na nje ya nchi, kama Kongo DRC, Zambia, Malawi na Msumbiji.”

Alisema uzalishaji ukiongezeka, sekta ya mifugo inayochangia asilimia saba katika Pato la Taifa (GDP), itaongezeka ikiwemo sekta ya ndogo ya maziwa inayochangia asilimia 1.2.

Alisema tasnia ya maziwa, ina ng’ombe 1,950,000 kutoka 1,294,000 waliokuwapo 2018/19 na hivyo kuongeza uzalishaji wa maziwa kutoka lita bilioni 2.7 mwaka jana hadi lita 3.0 mwaka huu.

JESHI la Kujenga Taifa (JKT) na ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi