loader
Solskjaer aanza tambo

Solskjaer aanza tambo

Bao kali la Paul Pogba na Edison Cavani la ugenini linalomfanya sasa kuwa na mabao manne msimu huu yameipeleka Man United juu ya msimamo wa Ligi Kuu England baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Fulham.
 
Tambo zimeanza kwa kocha wa timu hiyo, Ole Gunnar Solskjaer mara baada ya ushindi huo akidai kuwa wachezaji wake wako vizuri kuanzia utimamu wa mwili na kiakili na namna wanavyojituma kwa maslahi ya klabu hiyo.
 
“Tumefanya vizuri katika michezo mingi migumu, hilo ndilo jambo kubwa ambalo naendelea kusisitiza kwa wachezaji kwamba tunahitaji kushinda michezo mingi, tumeonyesha mabadiliko akili za wachezaji zinaonyesha zinahitaji ushindi.”alisema Solskjaer.
 
Kocha huyo aliyewahi kuitumikia klabu hiyo kama mchezaji alisema amevutiwa na kiwango cha kiungo Paul Pogba ambaye amekuwa akiamua matokeo ya ushindi michezo ya mwisho ya timu hiyo.

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/d288cc6e0f755c4feb9e956f45c259b2.jpg

Klabu ya soka ya Chelsea imefikia muafaka ...

foto
Mwandishi: MANCHESTER, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi