loader
Dstv Habarileo  Mobile
JPM amlilia Martha Umbulla

JPM amlilia Martha Umbulla

Rais John Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa Spika Job Ndugai kufuatia kifo cha Mbunge wa Viti Maalum CCM, Martha Umbulla kilichotokea usiku wa kuamkia leo alhamisi Januari 21, 2021 nchini India.

Taarifa  ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, inaeleza kuwa, Rais Magufuli, amepokea kwa masikitiko makubwa  taarifa za mbunge huyo wa Viti Maalum Mkoa wa Manyara aliyekuwa India akipatiwa matibabu.

Rais Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai, familia ya marehemu, wabunge na wananchi wote wa Mkoa wa Manyara na wote walioguswa na kifo hicho.

“Umbulla alikuwa mpole, mchapakazi, na mpenda maendeleo. Nazikumbuka jitihada zake za uongozi akiwa Mkuu wa Wilaya na akiwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” amesema Rais Maguguli katika taarifa hiyo ya Msigwa.

Amewaombea wana familia wote wawe na moyo ya uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi kigumu cha majonzi na kumuombea Martha apumzike mahali pema peponi.

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi