loader
Dstv Habarileo  Mobile
Simba kujipima kwa Mazembe, Al Hilal

Simba kujipima kwa Mazembe, Al Hilal

KLABU ya Simba  imetambulisha  mashindano mapya ya Super  Cup, maalumu kwa kukiandaa kikosi chao na mechi za hatua ya  makundi  ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika mwezi ujao.

Mashindao  hayo ya Super Cup  yatashirikisha timu tatu,  Simba ambao ni wenyeji, Al-Hilal  ya Sudan na TP Mazembe ya DR Congo inayotarajiwa kuanza  Januari 27 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez alisema  mchezo wa ufunguzi kikosi cha Simba kitawakabili  Al Hilal Jumatano kuanzia saa 11:00 Jioni.

“Leo Simba inatangaza rasmi mashindano yanayoitwa Simba Super Cup na tumealika wageni timu ya kwanza TP Mazembe ya DR Congo, na Al Hilal ya Sudan, itaanza rasmi wiki ijayo siku ya Jumatano  mechi ya kwanza Simba dhidi ya Al Hilal,”alisema   Gonzalez.

Naye Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara alisema kwa mara nyingine wanaandika historia mpya kwa kuanzisha mashindano kwa kuwashirikisha mabingwa  waliofanya vyema kwenye ligi za nchi zao na wanashiriki kimataifa.

Alisema matarajio yao benchi la ufundi watatumia michuano hiyo kutengeneza  utimamu wa mwili ya wachezaji wao  kuelekea kwenye michezo ya Ligi ya mabingwa inayotarajiwa kuanza Februari 12  ambapo Simba wataanzia ugenini dhidi ya  As Vita ya DR Congo.

Alisema mashindano hayo  timu zote zitatumia vikosi vyao vya kwanza  na malengo yao kama timu watapambana kuhakikisha wanabakisha kombe hilo ambalo wanaamini linaandika historia.

Pia Manara alisema timu za Tp Mazembe na Al Hilal zinatarajiwa kuanza kuwasili nchini Januari 26 kuanza maandalizi kwa michezo hiyo ambayo kilele kitakuwa Januari 31 ambapo Simba watacheza na TP Mazembe.

Pia alisema leo wataanza kutaja benchi la ufundi la timu hiyo akiwemo kocha wao mkuu baada ya kuondoka kwa Sven Vanderbroeck aliyejiunga na klabu ya ASFAR Rabat ya Morocco.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/e90383be34b0d2ee93264c8ff1253f36.jpg

TIMU ya Taifa ya Soka la Watu wenye ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi