loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

RPC Shinyanga ataka sheria ndogo kudhibiti ndoa, mimba za utotoni

KAMANDA wa polisi mkoani Shinyanga, Debora Magiligimba amemshauri mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kutunga sheria ndogondogo kuanzia ngazi za vijiji na kata kwa ajili kudhibiti ndoa na mimba za utotoni.

Magiligimba aliyasema hayo jana alipokuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa masuala ya ukatili waliokutanisha mashirika na asasi zisizokuwa za kiserikali katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ambapo wamekuwa wakitekeleza kupinga ukatili wa aina mbalimbali.

Alimshauri mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Hoja Mahiba kutunga sheria ndogondogo kuanzia ngazi za vijiji na kata kwaajili kudhibiti ndoa na mimba za utotoni kwani vitendo hivi vimeshamiri.

“Mkitunga sheria ndogondogo mtasaidia kupunguza mimba na ndoa za utotoni hata kuwakamata watuhumiwa kwani vitendo hivi vinafanywa na ndugu wa karibu kwa asilimia kubwa na wazazi wamekuwa hawawajibiki katika jukumu la malezi ya watoto wao,” alisema.

Magiligimba alisema kuwa wanawake na watoto ndiyo wamekuwa wahanga wakubwa dhidi ya vitendo vya ukatili kwani ukisha mfanyia kitendo hicho unamsababishia umasikini kwanza atataumia muda mwingi kufuatilia kesi, kupata ulemavu wa kudumu na kuathirika kisaikolojia.

Kamanda Magiligimba alisema kuwa vituo vya kusikiliza watu wanaofanyiwa ukatili (one step center) nchini viko katika mikoa minne ikiwemo Shinyanga na kuwa vina wataalamu walisomea kusikiliza vitendo hivyo na kitaifa unaisha na kufikia mwaka 2023 vitendo hivyo vinakuwa vimekiwsha kwa kutekelezwa mambo nane yaliyoainishwa.

Katibu wa mpango mkakati wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (Mtakuwwa) katika halmashauri hiyo Aisha Omary alisema kuwa wamepata jumla ya Sh millioni 25 na watatekeleza katika kata 13 kwa lengo la kutokomeza vitendo vya ukatili.

Mratibu wa WFT kutoka mkoani Shinyanga Grory Mbia alisema kuwa mradi huo umejikita zaidi katika masuala ya utafiti dhidi ya ukatili hivyo aliitaka halmashauri kuwapatia takwimu kwani uendeshaji wa shughuli bila kujua ukubwa wa tatizo inakuwa ni changamoto kwa wanaotekeleza.

MKUU wa Mkoa (RC)  wa Mwanza, ...

foto
Mwandishi: Kareny Masasy, Shinyanga

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi