loader
Dstv Habarileo  Mobile
City yapata pigo ity yapata pigo kwa de Bruyne

City yapata pigo ity yapata pigo kwa de Bruyne

KIUNGO wa Manchester City, Kevin de Bruyne atakaa nje ya uwanja kwa takribani wiki sita kutokana na maumivu ya misuli ya paja, amesema kocha Pep Guardiola.

De Bruyne aliumia wakati wa mchezo dhidi ya Aston Villa ambao ulimalizika kwa kuibuka na ushindi wa bao 2-0. De Bruyne anaweza kukosa hadi mechi 10, pamoja na mechi ya mwisho ya 16 ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Borussia Monchengladbach Februari 24.

“Daktari alisema baada ya kumkagua De Bruyne atakaa nje kwa wiki nne hadi sita. Ni pigo kubwa, lakini tunapaswa kusonga mbele,” alisema Guardiola.

“Sisemi chochote ambacho mtu yeyote hajui ni bahati mbaya kwake na kwetu na tunapaswa kupata suluhisho kwa sababu kila mtu katika maisha yake anajitahidi katika hali tunayoishi na inabidi tubadilike.

“ Nyota huyo ndiye anayeoongoza kwa pasi za mwisho za mabao katika ligi kuu ya England ambapo hadi anaumia alikuwa ametengeneza nafasi 10.

City hawajafungwa katika michezo 16 kwenye mashindano yote, ikiwa ni pamoja na kushinda katika mechi zao zote tisa zilizopita, na wanashika nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu, wakiwa alama mbili nyuma ya Manchester United, lakini wakiwa na mchezo mkononi.

Pamoja na mechi ya Kombe la FA, De Bruyne pia atakosa mechi za Ligi Kuu dhidi ya West Brom, Sheffield United na Burnley, Liverpool Februari 7 huko Anfield na Tottenham nyumbani siku sita baadaye.

Anaweza pia kutokuwepo kwenye mchezo dhidi ya Arsenal, mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Monchengladbach na mechi ya Ligi Kuu na West Ham.

City imepangwa kucheza mchezo wa watani wa jadi dhidi ya Manchester United Machi 6. Guardiola alisema wachezaji wake wanalazimika kucheza mechi nyingi na wanaendelea kupata majeraha.

“Kudai watapona kwa miezi 11 wakati wanacheza kila siku tatu, haiwezekani,” alisema. “Kwa mashindano haya, mwili unasema inatosha na wachezaji hawataki kuumia.

“Tunapodai kubadili hadi wachezaji watano, ni kwa sababu hii. Kwa nini tunafanya kwenye Kombe la FA lakini sio mashindano mengine? Sisemi tu kwa sababu ni Kevin, ni michezo na mashindano mengi na mwishowe wachezaji wanateseka,”

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/cde0458ad10da15506ff72a13ffcb4d7.jpg

Mambo yamaenza kuvurugika kunako klabu ya PSG, baada ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi