loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Uongozi MKURABITA kufanya ziara nyanda za juu kusini

Mkurugenzi Mtendaji wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara Tanzania (MKURABITA) Dk Seraphia Mgembe amesema kamati ya uongozi ya mpango huo itaanza ziara kwa ajili ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa shughuli za urasimishaji wa ardhi na biashara katika mikoa ya nyanda za juu kusini.

 Dk Mgembe amebainisha hayo Jijini Dodoma na kusema kuwa ziara hiyo inaanza leo na kukamilika Januari 31.2021.

“Kamati yetu itashiriki katika kazi mbalimbali ikiwemo zoezi la utoaji hati za hakimiliki za kimila na kumiliki Ardhi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa pamoja na kuweka jiwe la msingi la jengo la ofisi ya masijala ya ardhi katika Kijiji cha Kapya wilayani Mbarali mkoani Mbeya” amesema Mgembe.

MADEREVA nchini wametakiwa kujiamini na kuchukua ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi