loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tanzania kuwaachia wafungwa wa Ethiopia

Rais Dk John Magufuli amemuhakikishia Rais wa Ethiopia Salhe-Work Zewde kuwa Tanzania ipo tayari kuwaruhusu kurudi Ethiopia wafungwa wapatao 1789 ambao waliingia nchini kinyume na sheria na kuhukumiwa kwa mujibu wa sheria za nchi.

Rais Dk Magufuli amebainisha hayo leo akiwa wilayani Chato mkoani Geita kwenye ziara ya siku moja ya kiongozi huyo.

Amesema kupitia mazungumzo waliyofanya wamefikia makubaliano ya kuwaruhusu wafungwa hao pasipo masharti yoyote kutokana na historia nzuri ya mahusiano baina ya nchi hizi mbili.

“Sisi tutawaruhusu waondoke ‘free’ na nimemueleza ( Rais Zedwe) kwakuwa shirika lao la ndege lina ndege za kutosha wanaweza kutumia baadhi ya ndege  za shirika hilo kuwachukua wafungwa wote ambao kuna wengine tayari wana miaka saba wanatumikia vifungo vyao katika magereza ya hapa nchini” amesema Dk Magufuli.

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, ...

foto
Mwandishi: Alfred Lukonge

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi