loader
Mourinho : Lampard kutimuliwa ni ukatili katika soka

Mourinho : Lampard kutimuliwa ni ukatili katika soka

Chelsea jana ilimtimua Frank Lampard baada ya miezi 18 kuwanoa ‘The Blues’ yenye maskani yake London; Lampard anasema: “Nimehuzunishwa kutokuwa na muda wa kutosha msimu huu ili kufanya mengi mazuri yenye mafanikio”; Thomas Tuchel anatajwa kuchukua nafasi ya Lampard.
 

Kocha wa Spurs, Jose Mourinho anaamini kitendo cha Chelsea kumfukuza Lampard ni ukatili katika soka la kisasa hasa kwa kuzingatia Lampard amewahi kumfundisha miaka kadhaa nyuma akiwa mchezaji wa kablu hiyo
 
“Siku zote sifurahii mwenzangu kupoteza kazi,”amesema Mourinho, “Frank sio tu nimewahi kufanya nae kazi, bali ni mtu muhimu kwenye kazi yangu, kwahiyo namuone huruma kufukuzwa kwake,”.
 
Maoni ya Mourinho yanajiri baada ya jana kujihakikisha ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Wycombe Wanderes unaowapeleka raundi ya tano ya Kombe la ‘FA’ ambapo sasa watakutana na Everton katika Uwanja wa Goodson Park Februari 10,2020.

 

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi