loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Rais Magufuli azindua Shamba la Miti Silayo

Rais Dk John Magufuli leo amezindua na kubadilisha jina Shamba la Miti Chato na kuliita Shamba la Miti Silayo kama kumbukumbu kutokana na kazi kubwa aliyofanya ya uhifadhi wa misitu hapa nchini.

Dk Magufuli amebainisha hayo wilayani Chato mkoani Geita kwenye uzinduzi wa shamba hilo lenye hekari 69,000.

“Ifike mahali watu wanapofanya kazi nzuri wakumbukwe kwa kazi zao tunapenda mashamba na vitu mbalimbali kuitwa majina ya wanasiasa kwahiyo Prof Dos Santos Silayo nafikiri mamlaka hayo ninayo kwamba shamba hili baada ya kuitwa Shamba la Miti Chato sasa litaitwa Shamba la Miti Silayo” amesema Dk Magufuli.

Dk Magufuli amesema ameamua kufanya hivyo  kuenzi kazi kubwa iliyofanywa na Prof Silayo ambaye ni Kamishana wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) pamoja na vijana maaskari ambao wameendelea kulinda rasilimali za misitu.

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, ...

foto
Mwandishi: Alfred Lukonge

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi