loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Rais Magufuli atoa anagalizo chanjo ya Corona

Rais Dk John Magufuli ameitaka Wizara ya Afya kuacha kukimbilia chanjo ya virusi vya corona pasipo kujiridhisha ubora wa chanjo hiyo kabla ya matumizi kwakuwa inaweza kuwa na madhara.

Akizungumza kabla ya uzinduzi wa Shamba la Miti la Silayo, Dk Magufuli amewataka watanzania kuchukua taadhari zote za kiafya katika kukabiliana na ugonjwa huo ikiwa na pamoja na kujifukiza na kumwomba Mungu.

Dk Magufuli amesema hategemei kutangaza watu kujifungia ndani ‘Lock down’ kutokana na tahadhari ya virusi vya corona kwakuwa Mungu yupo na ataendelea kuwalinda watanzania.

“Mtatishwa sana ndugu zangu lakini simameni imara ninajua wapo baadhi ya watanzania wameondoka ndani ya nchi na kukimbilia maeneo mengine na kwenda kuchanjwa  na walipochanjwa huko wamerudi huku wametuletea Corona ya ajabu ajabu nawaomba msimame imara” amesema Dk Magufuli.

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, ...

foto
Mwandishi: Alfred Lukonge

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi