loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Rais Magufuli ampa miezi saba Kalemani

Rais, Dk John Magufuli amemuagiza Waziri wa Nishati, Medard Kalemani kuhakikisha ifikapo mwezi wa saba mwaka huu, kiwanda cha ‘Kom Group of Companies’ kitakapoanza kufanya kazi umeme haukatiki hata siku moja.

Dk Magufuli amebainisha hayo leo wilayani Kahama  mkoani Shinyanga mara baada ya kumaliza shughuli ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Kiwanda cha Kom Group of Companies.

“Kukatika umeme ni kujichelewesha maendeleo tuna umeme wa kutosha sasa hivi nchi tuna megawati za kutosha sasa ni jukumu la Wizara kupanga mikakati, saa nyingine tunazungumza mno ni lazima tutatue tatizo hili la kukatika umeme kabla ya mwezi wa saba” amesema Dk Magufuli.

Awali akizungumza katika tukio hilo Waziri wa Viwanda na Biashara Waziri wa Viwanda na Biashara, Geoffrey Mwambe amesema kuwa  msingi mkuu wa nchi ni kuwa na viwanda vingi hasa vile vinavyofungamana na sekta ya kilimo ili wakulima wapate soko la uhakika.

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, ...

foto
Mwandishi: Alfred Lukonge

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi