loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Rais Magufuli aipa hadhi Kahama kuwa Manispaa

Rais, Dk John Magufuli ameipandisha hadhi Halmashauri ya Mji wa Kahama mkoani Shinyanga kuwa Manispaa.
 
Dk Magufuli amefikia uamuzi huo leo wakati akizungumza na wananchi wa Kahama, baada ya kuvutiwa na namna nzuri ya ukusanyaji wa mapato na mipango mikubwa inayofanywa na viongozi wa manispaa hiyo katika kuleta maendeleo ya taifa.
 
"Nina sababu za msingi za kupandisha kwanza mapato, katika mkoa mzima wa Shinyanga wanachangia asilimia 50, hata makusanyo ya mapato ni miongoni mwa halmashauri chache katika nchi hii zinazoongoza katika makusanyo ya mapato,” amesema Dk Magufuli.
 
Aidha, Dk Magufuli amemsamehe mkurugenzi wa manispaa hiyo, Underson Msumba aliyenunua gari lenye thamani ya Shilingi milioni 400 pasipo kufuata taratibu za manunuzi.
 
“Nimeamua kumsamehe mkurugenzi huyu na hili gari ninamrudishia lakini asirudie tena kununua magari nje ya utaratibu wa sheria, nasema kwa dhati na sitaki kuwa mnafiki amefanya mambo makubwa ninajua unapigwa vita wanaokupiga vita sasa wakuogope unafanya kazi nzuri” amesema Dk Magufuli.

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, ...

foto
Mwandishi: Alfred Lukonge

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi