loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Rais Magufuli kuboresha maslahi ya watumishi wa afya

Rais, Dk John Magufuli ameahidi kuwa serikali itaboresha maslahi ya watumishi wa afya huku akiwataka kufanya kazi kwa bidii kwa kutanguliza uzalendo.

Dk Magufuli ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wananchi pamoja na watumishi wa afya mara baada ya kuweka wa jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la magonjwa ya dharura katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora.

Uamuzi huo umekuja mara baada ya kupewa taarifa kuwa kuna madaktari wameondoka licha ya kupangiwa kazi hospitalini hapo kwa madai ya kutoridika na kiwango mishahara.

"Tumeanza na hivi, baadaye tunaingia kwenye maslahi ya mtumishi wa afya, tunajua wanafanya kazi kubwa sana ya kujitolea," amesema Dk Magufuli.

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, ...

foto
Mwandishi: Rahimu Fadhili

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi