loader
Dstv Habarileo  Mobile
Kilio cha mwanamke chamgusa JPM Bahi

Kilio cha mwanamke chamgusa JPM Bahi

RAIS John Magufuli ameiagiza Halmashauri ya wilaya ya Bahi, mkoani Dodoma kumpa mwanamke, 59, shamba lenye ukubwa wa ekari tano ili  apande mikorosho na mazao mengine.

Mwanamke huyo ambaye jina lake halikuweza kupatikana alimlalamikia Rais Magufuli kwa kuwa alinyang’anywa shamba lao la kikundi ambacho kilikuwa na wanachama 72 bila fidia yoyote licha ya kuwasilisha kilio chao kwa Waziri mwenye dhamana ya ardhi.

 Baada ya kumsikiliza,  Rais Magufuli aliamuru Halmashauri ya Bahi kumpatia bure shamba la heka tatu mama huyo.

“Sheria ya Ardhi Namba 5....hata kama una plot (eneo)  lako la makazi na hujaendeleza unanyang’anywa, ila kwa heshima yako mama, naagiza DC na Mkurugenzi wa Halmashauri hii ya Bahi kumpa shamba ekari tatu mama huyu,” alisema Rais.

Baada ya agizo hilo,  Mkuu huyo wa nchi alimwambia mwanamke hiyo: “Mama nakupa heka tatu mlime mazao mengine na mpande mikorosho, nitakuja kuangalia kama mmetekeleza.”

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi