loader
Dstv Habarileo  Mobile
JPM awapa mtihani mzito Mbunge, viongozi Bahi

JPM awapa mtihani mzito Mbunge, viongozi Bahi

RAIS John Magufuli amemtaka Mbunge wa Bahi, Kenneth Nollo kushirikiana na mkuu wa wilaya hiyo na mkurugenzi halmashauri ya wilaya hiyo kubuni miradi ya maendeleo.

Rais Magufuli alitoa agizo hilo leo baada ya Mbunge wa Bahi, Kenneth Nollo kumuomba  kuipatia wilaya hiyo Sh milioni 70 ili iweze kujenga vituo 16 vya afya.

Mbunge huyo alisema wilaya ya Bahi ambayo ina changamoto mbalimbali ikiwamo maji, pia inakabiliwa na uhaba wa vituo 16 vya afya.

Hata hivyo, Rais Magufuli alimwambia Mbunge huyo hawezi kutoa tena fedha kwa ajili ya wilaya hiyo kwa kuwa sio wilaya pekee yenye changamoto.

“Nimetoa Sh milioni 150 kwa ajili ya kituo cha afya cha Mayamaya, mna bajeti ya serikali bilioni 28 hiyo hela ikalete impact, hii wilaya imetafunwa sana, imekuwa na mambo ya ajabu ajabu ndio maana niliwaondoa waliokuwepo, huyo Mkurugenzi na DC wa sasa hivi wanachapa kazi shirikiana nao mbuni miradi ambayo itawaletea maendeleo wana Bahi.”

“Kahama asilimia 50 ya miradi ya maendeleo inafanywa kwa mapato yao ya ndani na nyie fanyeni kazi, wilaya sio Bahi tu. Halmashauri hii ilikuwa inaliwa sana, Mbunge kasimamie fedha za wananchi nitakuwa nafuatilia, Dodoma na Bahi si mbali nitafuatilia maendeleo,” alisema Rais Magufuli.

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi