loader
Arteta: Arsenal ipo njia sahihi

Arteta: Arsenal ipo njia sahihi

MIKEL Arteta amesisitiza kuwa Arsenal inaelekea katika muelekeo sahihi baada ya kutoka suluhu dhidi ya Manchester United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.

The Gunners ambayo haikuwa na baadhi ya wachezaji wake muhimu kama Pierre-Emerick Aubameyang, Bukayo Saka na Kieran Tierney, ilikuwa na nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo dhidi ya kikosi cha kocha Ole Gunnar Solskjaer kwenye Uwanja wa Emirates.

Alexandre Lacazette nusura afunge baada ya shuti lake kugonga mwamba katika kipindi cha pili, wakati Emile Smith Rowe alishuhudia shuti lake likiokolewa na David de Gea na Nicolas Pepe akikaribia kufunga.

Hata hivyo, Arsenal ndio ilifaidika baada ya kuondoka na pointi moja ambayo imeshuhudia wakiendeleza rekodi la kutofungwa katika ligi na kufikia mechi saba.

Licha ya matokeo hayo, Arteta ambaye anaendelea kukiimarisha kikosi chake ambacho kilianza msimu vibaya, ameridhishwa na maendeleo ya sasa ya Arsenal. “Nafikiri yalikuwa matokeo ya haki.

Lilikuwa pambano kali kwa timu zote, kwa kweli timu zote zilikuwa zikihitaji kuibuka na ushindi.” “Makocha wote labda walifikiri wanaweza kushinda. Ulikuwa mchezo mgumu ambao tulicheza kwa nguvu zote.

Wachezaji wetu watatu wazuri tumewakosa katika mchezo huu labda hiyo ndio sababu. Lakini leo nina furaha kubwa na wachezaji wangu,” alisema Arteta. Wakati huohuo, beki Mbrazil wa Arsenal David Luiz amesema kocha Arteta ametengeneza timu nzuri katika mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Emirates baada ya timu yao kulazimisha sare dhidi ya Manchester United.

Vijana hao wa jiji la London walikuwa na nafasi nzuri ya kuibuka na ushindi huku wakiendeleza rekodi yao ya kutofungwa katika ligi hadi kufikia mechi saba sasa.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/7d44afd34aa6fc2d1fae07dba21d8297.jpg

PENALTI ya dakika za majeruhi iliyopigwa na mshambuliaji ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi