loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Rais Magufuli avutiwa ushujaa wa Jaji Galeba

Rais Dk John Magufuli amesema amefikia hatua ya kumteua Jaji Zepharine Galeba kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani kutokana na ujasiri na ushujaa wake wa kutoa hukumu katika moja ya kesi alizosimamia mwaka jana kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Dk Magufuli amebainisha hayo leo Jijini Dodoma kwenye hafla ya kumuapisha  Jaji huyo.

Aidha, Dk Magufuli amebainisha kuwa  utumiaji wa lugha ya kiingereza katika kuandika hukumu kwenye Mahakama za juu kunachangia kwa kiasi kikubwa kuwanyima haki watanzania wengi hasa wa hali ya chini kutokana na kutoimudu lugha hiyo ipasvyo.

“Kwa mujibu wa Katiba Mahakama ndio sehemu ya mwisho ya kufuatilia haki , haki inaweza kuchezewa kwingine huko kote lakini ikishafika mahakamani maana yake ndio mwisho sasa unapoona sehemu ndio mwisho na mtu kuandikiwa hukumu kwa lugha ambayo haijui kwa maoni yangu naona mahakama inashiriki mkumnyima haki huyo muhusika” amesema Dk Magufuli.

Awali akizungumza katika tukio hilo Jaji Zepharine Galeba amehaidi kuwatumikia wananchi kwa kutenda haki vile mwenyezu Mungu anavyotaka wanadamu waishi kwa kutenda haki.

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, ...

foto
Mwandishi: Alfred Lukonge

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi