Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) David Silinde amesema Serikali inatumia takwimu sahihi kwenye kukabiliana na upungufu wa madawati nchini kwa kuhakikisha kila madarasa mapya yanapojengwa inatengwa fedha kwa ajili ya madawati.
Silinde amebainisha hayo leo bungeni Jijini Dodoma kwenye kipindi cha maswali na majibu.
“Suala la upungufu wa madawati Serikali tunaendelea kupambana nalo pia wabunge tushiriki kama kuna changamoto sehemu mnaweza kutumia mfuko wa jimbo kufanikisha hilo huku tukishirikiana na wadau katika kukabiliana na tatizo hilo” amesema Silinde.