loader
Mndeme agoma kukabidhi madawati

Mndeme agoma kukabidhi madawati

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme amegoma kukabidhi madawati 50 na meza 10 za walimu katika Shule ya Msingi Mtakanini baada ya kutoridhishwa na ubora wa shule hiyo.
 

Mndeme amefikia hatua hiyo leo alipokwenda kuzindua vyumba viwili vya madarasa pamoja na samani hizo katika shule hiyo iliyopo wilayani Namtumbo.

“Madawati yameshavimba tayari hata wanafunzi hawajakalia, meza na viti zimeachia naomba mfanyie marekebisho vitu hivi ndio nije kukabidhi, mimi na akili zangu siwezi kukabidhi vitu vibaya kama hivi” amesema Mndeme.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi