loader
Silinde ataka Kambi ya Upinzani imuombe radhi JPM

Silinde ataka Kambi ya Upinzani imuombe radhi JPM

SAKATA la kukwama Katiba Mpya limeibuka tena bungeni ambapo Naibu Waziri wa Tamisemi, David Silinde amesema Kambi ya Upinzani inatakiwa kujilaumu yenyewe kwa kuingia mitini na inatakiwa kumwomba radhi Rais John Magufuli kwa kukimbia au kususia mjadala huo.

Hoja hiyo iliibuka wakati Bunge likijadili Hotuba ya Rais Magufuli aliyotoa Novemba 13, mwaka jana wakati akizindua Bunge la 12 jijini hapa. Silinde ambaye wakati huo alikuwa Kambi ya Upinzani, alikuwa akitoa taarifa kwa Mbunge wa Konde Khatib Issa Khatibu (ACT-Wazalendo), alisema Serikali ya CCM iliunda tume ambayo ilishughulikia mchakato wa kukusanya maoni.

“Lakini ngoma ilipokuwa nzito, sisi upande wa upinzani tukaingia mitini,” alisema Silinde. Silinde alisema hivyo si CCM iliyokwamisha mchakato huo, “bali ni sisi tuliokimbia ndani ya Bunge sababu ya kukwama hoja yetu ya kutaka Serikali Tatu.”

Aliongeza, “Malengo yalikuwa sahihi ya kujadili Katiba, lakini sisi tulikimbia Bunge, hivyo tumwombe radhi Rais atusamehe.”

Akiendelea na kuchangia hotuba ya JPM, Khatibu alisema kama Kambi ya Upinzani Chadema na CUF walikimbia hawakukimbia Watanzania, hivyo akaomba Rais Magufuli aendeleze mchakato huo kama alivyoahidi wakati akihutubia Bunge mwaka 2015 kwa manufaa ya Watanzania wote.

Mbunge wa Viti Maalumu, Anathropia Theonist (Chadema) aliomba serikali kumalizia kiporo cha kuandaa Katiba mpya na kwamba, wadau wake ni vyama vya siasa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na wanachama.

Mbunge wa Viti Maalumu, Agnes Mathew, alisema hakuna Katiba mpya bila maendeleo ndiyo maana Rais Magufuli alitumia Sh bilioni 400 zilizotengwa kukamisha mjadala kusaidia kusambaza huduma za jamii mfano maji, afya na nyingine.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/c7777254ef5c08c146a58a04b9f95164.jpg

WAFANYAKAZI wa Kituo cha Redio ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi