loader
Majaliwa aipa siku tatu TAMISEMI

Majaliwa aipa siku tatu TAMISEMI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameipa siku tatu Ofisi ya Rais –TAMISEMI kuhakikisha inafuatilia watumishi wa halmashauri zote zilizotakiwa kuhamia maeneo mapya lakini baadhi yao kushindwa kutekeleza agizo hilo.

Majaliwa amebainisha hayo leo bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Msukuma lililohoji juu ya utekelezaji wa agizo la rais Magufuli alilolitoa mwaka 2019, lililotaka halmashauri za vijijini zilizokuwa zinakaa mjini kuhama ndani ya siku 30 lakini hadi leo baadhi yao hawajafanya hivyo. 

“Nahitaji taarifa keshokutwa Jumamosi ofisini kwangu saa nne asubuhi ili nijue ni halmashauri gani bado watumishi wake hawajahama ili nichukue hatua nyingine za kinidhamu kwa watumishi hao” amesema Majaliwa.

Aidha, ameongeza kuwa hakuna haja ya watumishi hao kupewa muda mwingine na badala yake wanapaswa kuondoka kuanzia leo na kuwaagiza wakuu wa mikoa husika kuchukua hatua dhidi ya watumishi watakaokaidi agizo hilo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/5a5754b21c7718599fab64f181a50a60.jpg

RAIS Samia Suluhu Hassan amehutubia taifa ...

foto
Mwandishi: Alfred Lukonge

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi