loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Makosa yaliyopita yaijenge RT mpya

UCHAGUZI Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) ulifanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam na kupata viongozi wapya watakaokuwa madarakani kwa kipindi cha miaka minne ijayo.

Uchaguzi huo umefanyika kwa kutumia katiba mpya ya RT ambayo ilipitishwa hivi karibuni na ina mabadiliko mengi, ikiwemo utaratibu wa kuwapata wajumbe wa Kamati ya Utendaji na kuwepo kwa makamu mmoja wa rais badala ya wawili na mambo mengine kibao.

Kwa sasa wajumbe wa Kamati ya Utendaji wanapatikana kupitia Kanda sita na mmoja atakuwa akitokana na wanawake, ambaye yeye hana kanda tofauti na wengine sita.

MAKAMU WA RAIS

Huko nyuma kabla ya kubadilisha Katiba, RT ilikuwa na makamu wawili wa rais, makamu wa kwanza alikuwa akishughulikia utalawa ambaye ni William Kalaghe na wa pili alikuwa akishughulikia ufundi ambaye ni Dk Hamad Ndee.

Sasa makamu ni mmoja tu naye ni John Bayo, ambaye atakuwa akimsaidia kazi rais wa RT, Sailas Isangi.

Rais aliyepita wa RT pamoja na makamu wake, Anthony Mtaka na Kalaghe walienguliwa na Kamati ya Uchaguzi iliyoongozwa na mwenyekiti wake, Dk Jonas Tiboroha.

KAMATI YA UTENDAJI

Sasa wajumbe wa Kamati ya Utendaji wanatokea katika Kanda, hivyo tofauti na zamani, ambapo walikuwa wakichaguliwa kwa njia ya kawaida.

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji aliyeshinda kupitia Kanda ya Kati ni Michael Washa aliyepata kura 22, huku Kanda ya Kaskazini mshindi ni Alfred Shahanga aliyepata kura 13 wakati Kanda ya Magharibi mshindi ni Amon Mkoga aliyepata kura 18.

Mjumbe maalum wa wanawake ni Christina Panga aliyepata kura 13 na kumshinda Eva Gidabuday aliyepata kura tisa.

Wajumbe wa Kanda wako sita pamoja na yule aliyetokana na nafasi maalum ya wanawake jumla wanatakuwa wajumbe tisa badala ya awali walikuwepo 18.

WAWILI WAKUAJIRIWA

Katika uongozi mpya, kwa mujibu wa Katiba yao, Katibu Mkuu na Mhazini watakuwa wakiajiriwa, hivyo watakuwa na fursa ya kupatikana ofisini kila siku na wakatik wowote, kwani wakati wote wanatakiwa kupatikana ofisini na hilo ndio sababu ya kuwaahiri.

Hatua ya kuwaajiri wahusika hao kutasaidia RT kushughulikia mambao yao nay a watu wengine wakati wote kwani watu hao watakuwa wakifanya kazi kuanzia asubuhi hadi jioni ndani ya ofisi za RT.

UCHAGUZI UMEMALIZIKA

Uchaguzi una mambo mengi, yakiwemo makundi na fitina mbalimbali iki kila mtu anataka upande wake ndio ushinde na kuchukua ofisi.

Uchaguzi sasa umemalizika na uongozi ulioshinda unatakiwa kusahau yaliyopita na kufungua ukurasa mpya ili kutekeleza ahadi walizowaahidi wapiga kura wakati wa uchaguzi.

Uongozi mpya una mambo mengi ya kufanya kutokana na jinsi wenzao waliopita walivyovurunda wao wanatakiwa kuangalia nini walishindwa kukifanya au walideli wapi na wao ndio waanzie hapo.

Kwa kweli hakuna ubishi kuwa viongozi waliopita pamoja na kuwepo na mazuri waliyofanya, lakini asimilia kubwa walifeli kwani walishindwa kutekeleza kile ambacho kilitarajiwa na wengi kuleta maendeleo ua riadha.

Ukweli unabaki pale pale kuwa uongozi uliopita wa RT ulishindwa kabisa kuendeleza mchezo huo kitaifa na hata kimataifa, kwani Tanzania iliporomoka kabisa katika mchezo wa riadha.

VIKAO MUHIMU

Uongozi mpya uilioingia madarakani lazima ukumbuke kuwa vikao vya ndani kwa ndani ni muhimu sana pamoja na mikutano mkuu na mingine inasaidia kurekebisha matatizo yaliyokuwepo ndani ya shirikisho au katika mchezo kwa ujumla.

Ni jambo la ajabu uongozi uliopita ulishindwa kabisa kuendesha mikutano mikuu ya kila mwaka na hata vikao vya Kamati ya Utendaji, ambavyo shirikisho linatakiwa kufanya mikutano minne kwa mwaka, lakini RT walishindwa kabisa kuifanya.

Mkutani mkuu walitakiwa kuufanya kila mwaka, lakini katika kipindi cha miaka minne walishindwa kufanya hata mkutano mmoja na ndio maana walishindwa hata kurekebisha katiba hadi walipolazimishwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT).

Uongozi mpya unatakiwa kuangalia wenzao waliopita waliharibu wapi na wao ndio waanzie hapo na hilo ndoli litawasadia kufanya mambo vizuri na kuuendeleza mchezo huo kitaifa na kimataifa.

Dk. Hamad Ndee aliyekuwa makamu wa pili wa rais RT anakiri kuwa uongozi wao ulishindwa kabisa kutekeleza Katiba yao kwa upande wa vikao na mashindano ya taifa, ambayo badala yake walikuwa wakiendesha mashindano ya wazi, ambayo hayakuwa na nguvu.

Pia Dk Ndee anasema kuwa kwa ujumla wao, uongozi wote uliopita haukustahili kugombea tena, kwani haukuwa na sifa kwa kuwa ulishindwa kuuendeleza mchezo huo kitaifa na kimataifa.

Anasema kuwa kwa mtu mmoja mmoja wapo waliokuwa na sifa ya kuendelea kuongoza, lakini kiujumla hawakustahili kabisa kuendelea kushika nyadhifa katika uongozi wa sasa.

 Yote na yote, uongozi uliopo madarakani unatakiwa kuwa makini na kuhakikisha unafuata Katiba na kanuni za uendeshaji wa mchezo huo wa riadha.

Pia mbali na kuendeleza mchezo huo, uongozi uliopo madarakani unatakiwa pia kuangalia baadhi ya vipengele vya katiba iliyofanyiwa marekebisho ili kuvirekebisha kama kile cha wenyeviti wa mikoa kupiga kura, lakini havitoa nafasi kwa mtu mwingine kumuwakilisha endapo hatakuwepo.

 KUKABIDHI OFISI

Ni muhimu kwa uongozi uliopita kukabidhi ofisi kwa viongozi wapya pamoja na mambo mengine kama akaunti za benki, mali za shirikisho pamoja na wadhamini wanaoisaidia RT kama Benki ya NBC iliyoingia mkataba wa kuandaa NBC Dodoma Marathon.

 

RAIS Samia Suluhu ...

foto
Mwandishi: Cosmas Mlekani

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi