loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Bravo Simba, Namungo hatuwaelewi

KUNA wiki moja mbele kabla ya klabu za Simba na Namungo kuanza mechi zao za kimataifa Simba wapo katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Namungo wapo katika mzunguko wa pili wa Kombe la Shirikisho Afrika CAF.

Simba wamepangwa Kundi A, pamoja na timu za AS Vita kutoka DR Congo, Al Ahly ya Misri na Al Merreikh ya kule Sudan, wakati Namungo wamepangwa kucheza na Premeiro de Agosto ya Angola na endapo wataitoa watatinga hatua ya makundi.

Hiyo ni hatua nzuri sana kwa wawakilishi hao wa Tanzania lakini swali la msingi nikwamba wakati imebaki wiki hiyo moja kuna maandalizi ya msingi kwa timu hizo kwa ajili ya kufanya vizuri kwenye michuano hiyo au tunapeleka timu kimazoea kama ilivyozoeleka huko nyuma?.

Kwa upande wa Simba hakuna shaka kuanzia maandalizi yao pamoja na usajili walioufanya yanaleta matumaini ya kufanya vizuri kiasi fulani ukilinganisha na Namungo ambao hata maandalizi yao yamekuwa ya kawaida.

Simba imesajili wachezaji wenye uwezo na rekodi nzuri kwenye michuano iliyopo mbele yao, lakini pia waliandaa michuano maalumu ya Simba Super Cup, ambapo walizialika timu kubwa zenye rekodi ya kushiriki mara kwa mara michuano hiyo za TP Mazembe na Al Hilal ya Sudan.

Katika michuano hiyo, Simba iliibuka mabingwa mchezo wa kwanza wakiifunga Al Hilal ya Sudan mabao 4-1 na mchezo wa pili wakaenda sare ya bila kufungana na TP Mazembe na kufanikiwa kutwaa ubingwa kwa kufikisha pointi nne ambazo hazikufikiwa na timu mbili za Mazembe na Al Hilal.

Ukiachilia mbali matokeo na ubingwa, unaweza kusema Simba imefaidika kutokana na kipimo kizuri kutoka kwa miamba hao wa Afrika na sasa wanaelekea kwenye michuano hiyo wakijua ubora na udhaifu wa timu yao tofauti na Namungo ambao wamekuwa kimya.

Namungo ukiacha usajili wa mshambuliaji Patrick Kwizera hakuna ingizo jipya ambalo unaweza kusema linakwenda kuongeza changamoto kwa wachezaji wa kikosi hicho hasa ukizingatia timu wanayokwenda kukutana nayo hivi sasa ni tofauti ukilinganisha na zile za Sudan ambazo walicheza nazo hatua ya awali na mzunguko wa kwanza.

Bado haijaeleweka nini sababu ya Namungo kuwa kimya bila kufanya maandalizi ya kuwakabili waangola hao kwani ni miongoni mwa timu ambayo imebeba matumaini makubwa ya Watanzania katika michuano hiyo kwani kufanya vizuri kwa timu hizo mbili kunafaida kwa taifa la Tanzania.

Faida ni endapo timu hizo zitafanya vizuri na kutinga hatua ya robo fainali kuna uwezekano mkubwa msimu ujao Tanzania ikipeleka timu nne kwenye michuano ya kimataifa kwa maana timu mbili kwenye Ligi ya Mabingwa na mbili nyingine kwenye Kombe la Shirikisho Caf.

Inavyoelekea Namungo tayari wameyapima maji na kubaini kwamba siyo saizi yao na sasa wameacha kufanya maandalizi kabambe ili kupata visingizio endapo itatokea wakatolewa lakini hilo halitokuwa na mantiki kwao na taifa kwa ujumla lakini hongera yao Simba kwa maandalizi mazuri hata ikitokea wameshindwa kuvuka hatua ya robo fainali hakuna atakayewalaumu sababu tayari wameonyesha nia.

RAIS Samia Suluhu ...

foto
Mwandishi: Mohammed Akida

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi