loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Suala la Tambwe liwe fundisho kwa klabu zote

WIKI hii kumekuwa na taarifa za Yanga kutakiwa kumlipa mchezaji wake wa zamani Amisi Tambwe ama ifungiwe kusajili kwa miaka mitatu.

Tambwe anaidai Yanga Sh milioni 41 walizotakiwa kumlipa baada ya kutohitaji tena huduma yake takriban misimu miwili iliyopita.

Taarifa za suala hilo zimetoka Shirikisho la soka la kimataifa, Fifa na Yanga tayari wako kwenye mchakato wa kulipa deni hilo.

Tambwe sio wa kwanza kuidai Yanga, wapo wachezaji wengine kadhaa wanaidai timu hiyo, pia wapo baadhi ya makocha ambao mara kwa mara kwa nyakati tofauti wamewalalamikia mabingwa hao wa kihistoria wa Ligi Kuu Bara kuhusu stahiki zao.

Si jambo zuri kwa afya ya mpira wa nchi, tunatoa ushauri kwa viongozi kufanya kazi zao inavyotakiwa badala ya kuchukulia mambo juujuu.

Tunasema hivyo kwa sababu kama Yanga leo ingelipa deni hilo mapema kusingekuwa na habari za kutishiana kufungiwa usajili.

Ujumbe wa viongozi kutimiza majukumu yao si kwa Yanga tu, hii ni kwa timu zote na majukumu hayo yatimizwe kwa wachezaji wote si wa kigeni tu hata wazawa kwani nao mara kwa mara wamekuwa akilalamikia kunyimwa stahiki zao.

Viongozi wa soka wanatakiwa kufahamu kuwa mpira ni ajira hivyo ni lazima vipengele vya mkataba wanaoingia na wachezaji vitimizwe, ikiwemo malipo, wajue wachezaji nao wana familia zao zinawategemea.

Tunaimani Yanga itamaliza suala hilo na klabu nyingine zitajifunza na hilo halitajirudia tena.

RIPOTI ya 15 kuhusu uchumi wa Tanzania ya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi