Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amesema timu hiyo haipaswi kuchukuliwa kama moja ya timu zinazoweza kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL) mara baada ya kutoka sare ya 3-3 dhidi ya Everton.
“Hatutakiwi kuchukuliwa kama timu inayoweza kushinda taji, tumetoka mbali sana hadi sasa kuwa katika kiwango hiki tunachokionesha lazima tufanyie kazi tatizo la kuruhusu kufungwa magoli rahisi” amesema Solskjaer.
Kufuatia sare hiyo Manchester United imepoteza nafasi ya kukaa kileleni mwa ligi hiyo dhidi ya mahasimu wao Manchester City ambao wana michezo miwili mkononi.