loader
Dstv Habarileo  Mobile
Majaliwa : Sio utaratbu askari kumkimbiza bodaboda

Majaliwa : Sio utaratbu askari kumkimbiza bodaboda

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema sio utaratibu kwa askari polisi wa usalama  kumkimbiza mwendesha pikipiki maarufu kama ‘bodaboda’ anapofanya makosa na kwamba kuna utaratibu wa kuwawajibisha wanapovunja sheria za barabarani.

Majaliwa ameyasema hayo leo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalumu, Sylvia Sigula ambalo lilihoji juu ya mkakati wa Serikali katika kupunguza ajali zinazotokana na polisi kuwakimbiza madereva wa bodaboda.

Akijibu swali hilo, Majaliwa amesema hakuna utaratibu wa kuwakimbiza madereva bodaboda lakini sheria imeweka utaratibu wa ukaguzi pamoja na kuwaelimisha watumiaji wa vyombo vya moto.

“Serikali imeweka utaratibu mzuri, wakurugenzi wa halmashauri wamepewa maelekezo ya kuwapa elimu, kuwatengea maeneo katika maeneo yao. Hilo linafanyika katika maeneo mbalimbali,” amesema Majaliwa.

Amewataka madereva wote wa vyombo vya moto na jeshi la polisi kufuata sheria katika usimamizi ili kuepusha ajali zinazoweza kutokea hasa pale polisi wanapowafukuza waendesha bodaboda.

foto
Mwandishi: Rahimu Fadhili

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi