loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Rais Magufuli amuagiza Jafo kusimamia urudishwaji wa fedha

Rais Dk John Magufuli leo amemuagiza Waziri wa TAMISEMI, Suleiman Jafo kusimamia watendaji wote wa Manispaa ya Morogoro wenye vizimba katika Soko Kuu kurudisha fedha yote ya ziada waliyokuwa wanawatoza wananchi katika soko hilo.

Akizungumza katika uzinduzi wa soko hilo, Dk Magufuli alisema ujenzi wa soko hilo umegharimu zaidi ya Shilingi bilioni 17 lengo likiwa kuwasaidia wananchi wa hali ya chini hivyo wanapojitokeza watu kama hao wanaochukuwa kamisheni kwenye vizimba vya wafanyabiashara vitendo kama hivyo havikubaliki.

“Wafanyakazi wote wa Manispaa wenye vizimba awe mfanyakazi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa au Ofisi ya Mkuu wa Wilaya au mfanyakazi wa Manispaa au mfanyakazi sijuhi nani nataka waziteme fedha zote walizozichukua kama kweli wanapenda kazi zao” amesema Dk Magufuli.

Katika hatua nyingine Dk Magufuli ametangaza soko hilo kuitwa Soko la Kingali kama njia mojawapo ya kumuenzi kiongozi huyo wa kimila aliyefanya mambo mengi makubwa kwenye shughuli za utunzaji wa mazingira.

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, ...

foto
Mwandishi: Alfred Lukonge

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi