loader
Mourinho ashangaa majeraha ya Bale

Mourinho ashangaa majeraha ya Bale

JOSE Mourinho amesema ameshangazwa na majeraha ya sasa ya Gareth Bale yaliyomuweka nje mchezaji huyo wa Wales kwenye kikosi cha Tottenham. 

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 anayecheza kwa mkopo bado anaandamwa na jinamizi la majeraha alilotoka nalo Real Madrid.

Bale hakujumuishwa kwenye kikosi cha Spurs kilichofungwa 5-4 kwenye raundi ya tano ya kombe la FA dhidi ya Everton. Mourinho amebainisha kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Wales aliomba kufanyiwa uchunguzi na kujiondoa mwenyewe kikosini. 

 “Nadhani ni vema kwangu kusema tulicheza na West Brom Jumapili hakucheza alikuwa benchi,” alisema Mourinho akiwaambia waandishi wa habari kuhusu Bale.

“Jumatatu nilishangazwa alipotaka kufanyiwa uchunguzi kwa vile alihisi hayuko sawa.”

“Hakufanya mazoezi Jumatatu, Jumanne alifanya mazoezi na timu lakini niliambiwa bado ameamua kufanya na wataalamu wa afya kwa vile anahisi hayuko vizuri.”

“Hiyo ndio sababu kwanini hayuko hapa, sidhani kama ni majeraha ya kawaida.”

Tottenham imecheza mechi 38 kwenye michuano yote msimu huu. 

Bale amekuwa akiandamwa na majeraha kwa miaka ya karibuni na hiyo ni moja ya sababu zilizomfanya kushindwa kuwa kwenye kikosi cha Zinedine Zidane Real Madrid.

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi