loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Rais Magufuli aagiza maboresho ya nembo Kiwanda cha Mpunga

Rais Dk John Magufuli amekitaka Kiwanda cha Mpunga cha Murzar Wilmar kilichopo mkoani Morogoro kutengeneza nembo nyingine katika mojawapo ya bidhaa inazozalisha kuwa na jina linalohusu Tanzania kama njia mojawapo ya kuitangaza nchi yetu.

Dk Magufuli amebainisha hayo leo Ijumaa alipokuwa anazindua kuwanda hicho mkoani humo chenye uwezo wa kukoboa tani 280 za Mpunga kwa siku.

“Sasa kwasababu mchele huu umetoka kwa wakulima kutoka Tanzania siwazuii kuendelea kuendelea kutumia nembo yenu ya Korie lakini pawe na ‘Brand’ nyingine inayotangaza Tanzania   hiyo itakuwa njia mojawapo ya kuitangazaa nchi yetu” amesema Dk Magufuli.

Dk Magufuli amesema kuna bidhaa nyingi  zenye ubora zinatoka hapa nchini yakiwemo maparachichi na nyama lakini zimebandikwa nembo  kutoka nchi nyingine  kitu kinachorudisha nyuma nchi yetu kujitangaza kwenye suala la uzalishaji.

 

 

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, ...

foto
Mwandishi: Alfred Lukonge

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi