loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ngorongoro yaenda Mauritania

KIKOSI cha wachezaji 29 cha  timu ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes kimeenda Mauritania kushiriki mashindano ya Mataifa ya Afrika (Afcon) yanayotarajiwa kuanza kesho.

Michuano hiyo itashirikisha mataifa 12 yaliyofuzu kutoka kanda tofauti ambapo kwa upande wa Afrika Mashariki itawakilishwa na Tanzania na Uganda.

Nahodha wa kikosi hicho, Kelvin John alisema wanataka kuweka historia katika michuano hiyo kwa kuhakikisha kila mchezo wanapambana kwa uwezo wao kupata pointi tatu.

“Kila mchezaji ana shauku ya kufanya makubwa tutahakikisha tunaitetea nchi yetu tutapambana kwa kila mchezo tuweze kupata matokeo ya ushindi,”alisema.

Kocha Mkuu wa Ngorongoro, Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ alisema kwa maandalizi mazuri ambayo kikosi chake imefanya kwa muda mrefu wameonesha mwanga kuwa wanaweza kuonesha kitu kwenye michuano hiyo.

“Mechi nyingi za kirafiki tulizocheza zimeonesha kuwa kuna kitu tunaweza kufanya kwasababu kila mchezo, walikuwa wanaonekana kubadilika na kuimarika, tunaweza kufanya kitu Afcon,”alisema.

Ngorongoro inayoshiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza, itacheza mchezo wake wa kwanza Jumanne dhidi ya Ghana.

Timu nyingine zilizopo Kundi C ni  Gambia na Morocco ambazo Tanzania itakuja kucheza nazo baada ya mchezo huo wa kwanza.

LICHA ya Simba kumaliza michezo ya ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi