loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Robo fainali FA kuchezwa Machi

ROBO Fainali ya Kombe la FA inatarajiwa kuchezwa Machi 20-21, ambapo Bournemouth watakuwa wenyeji wa Southampton, Chelsea itacheza na Sheffield United.

Everton watawakaribisha vinara wa Ligi ya England, Manchester City kwenye Uwanja wa Goodison Park, wakati Manchester United watasafiri kuifuata Leicester.

Chelsea ambayo ilifuzu baada kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Barnsley uliochezwa Alhamisi iliyopita watakuwa nyumbani kucheza na Sheffield United inayoburuza mkia kwenye Ligi Kuu England.

Bournemouth wanaoshiriki Championship ambayo sasa inatafuta kocha mpya wa kudumu watacheza dhidi ya Southampton.

Everton ilifikia robo fainali miaka nane iliyopita baada ya kucheza mchezo wa kusisimua wenye mabao tisa dhidi ya Tottenham Jumatano iliyopita, huku muda wa nyongeza Bernard akiwapa ushindi wa 5-4 dhidi ya kikosi cha Jose Mourinho.

City, wakati huo huo, iliweka historia ya mpira wa miguu England kwa kuvunja rekodi ya ushindi mfululizo (15) katika mashindano yote na timu iliyo juu wakati walipowachapa Swansea 3-1 katika raundi ya tano Jumatano iliyopita.

Everton watakabiliana na City baada ya mechi ya awali ya ligi Desemba 23 kuahirishwa kufuatia kikosi cha City kukutwa na corona.

Mechi hiyo imepangwa kufanyika Februari 17.

Leicester na United zilikutana kwenye Ligi Kuu Desemba 26 mwaka jana, wakati Axel Tuanzebe alijifunga dakika ya 85 lilifanya Mbweha hao kutoka sare ya 2-2 huko King Power.

Timu hizi zinatofautiana kwa pointi mbili tu kwa sasa kwenye msimamo wa ligi baada ya michezo 23, huku United ikishika nafasi ya pili na Leicester ya tatu.

LICHA ya Simba kumaliza michezo ya ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi