loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Klopp: Sisikilizi kelele

KOCHA Jurgen Klopp amesema hasikilizi ‘kelele’ zinazotokana na Liverpool kushuka lakini ‘anajali’kiwango chao  fomu yao.

Wekundu hao wanaoshika nafasi ya nne, ambao wamecheza mchezo mmoja zaidi, wanazidiwa kwa pointi 10 na vinara Manchester City.

Wameshindwa michezo miwili iliyopita lakini watasonga juu ya Leicester ikiwa walishinda mchezo wa jana.

"Tunayo michezo 15, ni pointi nyingi. Sio juu ya wengine wako wapi au wanaishia wapi. Inatuhusu sisi tu," alisema Klopp.

Licha ya kushinda Ligi Kuu kwa alama 18 msimu uliopita, wastani wa pointi za Liverpool kwa kila mchezo imeshuka zaidi kuliko timu nyingine yoyote ya Ligi Kuu tangu michezo ilipoanza kuchezwa bila ya mashabiki Juni mwaka jana.

Wekundu hao wamekumbwa na majeraha mabaya kwa wachezaji wakiwemo mabeki Virgil van Dijk, Joe Gomez na Joel Matip.

Mshambuliaji Mreno Diogo Jota, ambaye amefunga mabao tisa katika michezo 17 tangu uhamisho wake wa pauni milioni 41 kutoka Wolves Septemba iliyopita, hajacheza tangu Desemba 9 kwa sababu ya jeraha.

Klopp aliongeza: "Tunajua tunapaswa kufanikiwa siku za usoni na ndivyo tutakajaribu kuwa.

"Sisikilizi kelele kwa sababu ya matokeo. Chochote ulichoandika, sikusoma. Lakini najua hali ilivyo na ninazungumza juu ya matokeo.

"Ingawa ninajua sababu ya kutosafiri, ninatarajia tushinde michezo mingi kuliko tuliyo nayo.

"Tutajitahidi kufanya msimu bora kuanzia sasa. Tutafanya hivyo. Hiyo ni kazi yetu."

LICHA ya Simba kumaliza michezo ya ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi