loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Yanga yakwama Mbeya

YANGA imelazimishwa sare ya bao 1-1 ugenini na Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya jana.

Katika mchezo huo ambao ulikuwa wa ushindani ulishuhudia timu zote zikienda mapumziko bila kuona lango la mpinzani wake.

Sare hiyo inaifanya Yanga kufikisha pointi 45 ikiendelea kuwa kileleni lakini ikiwa Simba itashinda mechi zake mbili za kiporo atamfikia huku Mbeya City ikiendelea kuwa ya mwisho kwa pointi 15.

Yanga ndio iliyokuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 74 lililofungwa na Deus Kaseke aliyeingia kuchukua nafasi ya Fiston Abdulrazack.

Mbeya City ilisawazisha dakika ya 90 kwa penalti ambayo ilitokana na Yassin Mustapha wa Yanga kunawa mpira eneo la penalti wakati akiokoa na bao likafungwa na Pastory Athanas.

Yanga ilimiliki mpira kwa asilimia kubwa huku wapinzani wao wakionekana kucheza kwa kujihami na kulinda lango.

Mbeya City ilionesha wazi kuwa inataka sare kutokana na uchezaji wake katika dakika 90.

Hata hivyo Yanga walitengeneza nafasi nyingi ila hawakuweza kupenya kirahisi katika lango la wapinzani kutokana na ukuta kuwa imara.

Katika mchezo mwingine uliochezwa mapema, Biashara United ikiwa katika uwanja wa nyumbani, Karume, Mara iliifunga Mwadui kwa mabao 2-1 na kuifanya kufikisha poibti 32 katika nafasi ya nne na Mwadui ikishika mkia.

LICHA ya Simba kumaliza michezo ya ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi