loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mchezaji Ihefu atamba kuendelea kufunga

BAADA ya kikosi cha Ihefu kurejea kwenye michezo ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kupata ushindi, mshambuliaji wa timu hiyo, Issa Ngoah ametamba  kuendelea kuifungia timu yake mabao.

Ngoah aliifungia timu yake mabao yote kwenye mchezo ulioisha kwa Ihefu kuchomoza na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ruvu Shooting uliochezwa Uwanja wa Mabatini, Pwani juzi.

Akizungumza kutoka Pwani jana, Ngoah alisema kabla ya kuingia kwenye mchezo huo alipewa maelekezo na kocha wake, Zuberi Katwila kwamba anatakiwa kuwa makini kwenye eneo la mwisho kwakuwa wapinzani wao walikuwa wanafanya makosa mengi.

“Nilifuata maelekezo niliyopewa na kocha kwani kabla ya mchezo aliniambia wachezaji wanaocheza nafasi ya ulinzi kwa upande wa Ruvu Shooting kuna wakati wanajisahau na mimi niliongeza utulivu na kutimiza nilichoambiwa,” alisema. 

Ngoah amewaahidi mashabiki wa timu hiyo kuendelea kufunga kwakuwa kikosi hicho hakipo nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi hiyo kwani wanashika nafasi ya 16 wakiwa na pointi 16 baada ya kucheza michezo 19.

Katika mchezo huo ambao Ruvu Shooting walitawala kwa kutengeneza nafasi nyingi za kufunga na kushindwa kuzitumia, ilishuhudia Ngoah akiweka wavuni mabao hayo dakika za 21 na 90 yote akitumia uzembe uliofanywa na safu ya ulinzi ya wapinzani.

Ihefu wanajipanga kwa mchezo unaokuja dhidi ya Mtibwa Sugar utakaochezwa keshokutwa kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro

LICHA ya Simba kumaliza michezo ya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi