loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Simba akili yote kwa Biashara

 SIMBA imerejea jana nchini kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na kocha wake, Didier Gomes amesema akili yake yote ni kupata ushindi dhidi ya Biashara United kwenye mechi ya Ligi Kuu Alhamisi ya wiki hii.

Wawakilishi hao wa Tanzania kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa wameanza vema hatua ya makundi ya michuano hiyo baada ya kushinda bao 1-0 dhidi ya AS Vita ya DRC mwishoni mwa wiki iliyopita.

Akizungumza muda mfupi baada ya kuwasili Dar es Salaam jana, Gomes alisema amejipanga kuwapa mbinu za ushindi wachezaji wake katika mechi na Bishara. 

Alisema hawana muda wa kufurahia ushindi wa Vita bali wanawaza mechi iliyo mbele yao ambayo ana amini itakuwa ngumu.

Mechi ya mzunguko wa kwanza Simba ilishinda mabao 4-0 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam. 

“Mchezo unaokuja utakuwa mgumu na tunahitaji ushindi pia kwakuwa tupo kwenye ratiba ngumu, Biashara ni timu ngumu kama nyingine zinazoshiriki ligi hivyo tunahitaji kufanya maandalizi ya kutosha na hatuwezi kuwadharau wapinzani wetu,” alisema.

Gomes alisema wachezaji wake baada ya kuwasili jana aliwapa mapumziko ya siku moja na leo wanatakiwa kuingia kambini tayari kwa maandalizi ya mchezo huo ambapo kesho watafunga safari ya kwenda Mwanza kabla ya kuunganisha Musoma. 

“Mchezo huo tunahitaji ushindi kuongeza morali kwa wachezaji kujipanga na mchezo dhidi ya Al Ahly ya Misri mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakao chezwa hapa nyumbani,” alisema Gomes.

Alisema baadhi ya wachezaji wake wamechoka na wengine wameumia kutokana na ushindani walioupata kwenye mchezo uliopita dhidi ya As Vita lakini anawapongeza kwa kucheza kwa nidhamu katika mechi hiyo.

LICHA ya Simba kumaliza michezo ya ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi