loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Dodoma Jiji yaizamisha JKT

DODOMA Jiji FC ilijihakikishia pointi tatu baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya JKT Tanzania kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Jamhuri,  Dodoma jana.

Wenyeji Dodoma  walipata ushindi kwa mabao yaliyowekwa kimiani na Khamis Mcha dakika ya tisa, bao la pili likipachikwa na Anuary Jabir dakika ya 81 huku wapinzani wao JKTwakipata bao la kufutia machozi dakika ya 51 na Edson Katanga. 

Ushindi huo umewafanya Dodoma Jiji kufikisha pointi 25 na kushika nafasi ya nane kwenye msimamo baada ya kucheza michezo 19 wakati wapinzani wao  JKT Tanzania wakisalia nafasi  14 na pointi 20 wakishuka uwanjani mara 19.

Katika mchezo huo haukuwa na ushindani mkubwa kutokana na mazingira ya uwanja huo kujaa matope  kwa baadhi ya maeneo  kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini.

Mchezo ulianza kwa kasi kwa timu zote kucheza mpira  wa kujihami zaidi na kushambuliana kwa zamu lakini kadri muda ulivyokwenda Dodoma walionekana kuwa bora.

Kipindi cha pili kilirejea kwa kasi kwa pande zote kufanya mabadiliko yaliyonekana kuwaongezea nguvu Dodoma eneo la kiungo waliendelea kutawala na kutengeneza mashambulizi kupitia pembeni.

KOCHA wa Simba, Didier Gomes na wa Yanga, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi