loader
Marekani Urusi zakubaliana upya kupunguza silaha kali

Marekani Urusi zakubaliana upya kupunguza silaha kali

MAREKANI na Urusi zimekubaliana kuongeza mkataba mpya wa kupunguza silaha kali za kimkakati, huku Marekani ikiangalia namna nyingine ya kuboresha utulivu wa kimkakati duniani.

Hayo yalibainishwa hivi karibuni na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken.

Alisema hapo zamani nchi hizo mbili hazikukubaliana katika suala hilo na Marekani ilikuwa na wasiwasi kuhusu tabia na matendo ya Urusi, lakini bado nchi hizo zinaweza kushirikiana katika maeneo ambayo wana maslahi nayo. 

“Tunaweza kwa haraka sana kwa sababu jambo hilo tuna maslahi nalo la kuongeza mkataba mpya wa miaka mitano kuhusu makubaliano ya kudhibiti upunguzaji wa silaha, kisha tutaona namna ya kuimarisha utulivu wa kimakakati na Urusi hata kama tunaelewa kuhusu hatua wanazochukua ambazo ni changamoto kwa maslahi na maadili yetu lakini lazima tufanya kazi pamoja,” alisema Blinken

Mkataba wa awali kati ya nchi hizo mbili wa kupunguza na kudhibiti silaha kali za kimkakati ulisainiwa mwaka 2010 na kuanza kutekelezwa Februari 5, 2011.

Mkataba huo pamoja na mambo mengine unasema kuwa, miaka saba baada ya kuanza utekelezaji kila upande unatakiwa usiwe na makombora zaidi ya 700 ya masafa marefu (ICBM), makombora ya masafa marefu ya manowari (SLBM) na mabomu ya kimkakati.

 

Urusi na Marekani zilibadilishana taarifa za kidiplomasia kuhusu makubaliano ya mkataba mpya Januari 26 na Februari 3 mwaka huu.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi na Ubalozi wa Marekani nchini humo zimebadilishana taarifa ya kukamilika kwa taratibu za ndani za kutekeleza makubaliano hayo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/341d2491189f489e437f5bf4ef408797.jpg

RAIS Mstaafu wa Awamu ya ...

foto
Mwandishi: WASHINGTON, Marekani

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi