loader
Mkuu wa Shule asimamishwa kazi  mradi kutokamilika

Mkuu wa Shule asimamishwa kazi  mradi kutokamilika

NAIBU Waziri wa Ofisi ya Rais Tamisemi, David Silinde amemsimamisha kazi Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Naliendele, Halidi Mchanga kwa kushindwa kukamilisha mradi wa bweni na bwalo la chakula .

Silinde amechukua uamuzi huo alipotembelea shule hiyo iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani na kukuta matumizi mabaya ya fedha za  ujenzi ambapo ulitakiwa kuwa umekamilika mwaka jana.

Katika hatua nyingine, Silinde amemuagiza Ofisa Elimu Sekondari wa Manispaa , Mayembe Mangula kuandika barua ya kujieleza kwa nini asichukuliwe hatua kali na kuvuliwa nyadhifa zake baada ya kushindwa kusimamia ujenzi huo.

“Nataka barua yako Tamisemi haraka ya kwa nini tusikuvue madaraka kwa kushindwa kusimamia ujenzi, Mtwara Mikindani mmekua wa mwisho kitaifa nchi nzima kwa kuharibu mradi huu,”alisema Silinde.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani, Emanuel Mwaigobeko alisema wataongeza fedha ili kukamilisha mradi wa bweni la wanafunzi mpaka kufikia Agosti mwishoni watakua wamekamilisha bweni hilo.

Katika utetezi wake kwa Silinde, Mkuu wa Shule ya Naliendele, Mchanga alisema walikutana na changamoto ya upatikanaji wa saruji, mvua kubwa kukwamisha ujenzi ikabidi wasubiri ziishe mwanzoni mwa mwaka huu na ushiriki hafifu wa wananchi katika kuchangia ujenzi ikiwa ni kuchimba msingi.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/32e0d051d2a7a2afdfc7dfec44374da2.png

WAFANYAKAZI wa Kituo cha Redio ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi