loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

HII ACHA

KOCHA wa Simba, Didier Gomes amesema wachezaji wake wataendeleza nidhamu ya kujilinda na kushambulia kwa kushtukiza kwenye mchezo wa pili wa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly  ya Misri unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam, Kesho jioni.

Simba wataingia kwenye mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya kutoka kuibuka na ushindi  bao 1-0 mchezo wa kwanza wa ugenini dhidi ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo sawa na Al Ahyl wanaongoza kundi hilo baada kuibuka na mabao 3-0 dhidi ya Al Merrikh ya Sudan.

Akizungumza  Dar es Salaam juzi, Gomes alisema  hakuna mchezo rahisi kwenye hatua hiyo nidhamu ya kumuheshimu mpinzani ni lazima.

“Tunaenda kucheza na Al Ahyl mabingwa watetezi wanawachezaji wenye mbinu na wanafanya vizuri, lakini kwetu tunayonafasi ya kujipanga kulinda ushindi sioni kama kunambinu zaidi ya kuongeza nidhamu katika kuzuia mashambulizi yao,”alisema Gomes

Alisema wachezaji wake wanaendelea vyema na uzuri wapo kwenye kipindi kizuri baada ya kuanza vyema ugenini na safari hii watakuwa nyumbani mipango yao ni kuendeleza wimbi la ushindi kujitengenezea mazingira mazuri kwenye kundi hilo.

Simba watacheza mchezo huo na Al Ahly ambao ni mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo wakiwa na kumbukumbu ya kutoka kuibuka na ushindi wa bao 1-0 kwenye mchezo wa hatua kama hiyo msimu wa mwaka juzi.

Naye Pitsone  Mosimane, Kocha Mkuu wa Al Ahly alisema kuwa kipigo chao cha bao 1-0 ambacho walikipata mbele ya Simba wamekifanyia kazi hivyo wataingia kwa tahadhari.

Tayari Kikosi cha wachezaji 22 wa Al Ahly ya Misri wapo nchini walitua Februari 19, 2021 usiku kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo huo huku ikitarajia kuwakosa nyota wao watano Ali Maaloul, Taher Mohamed Taher, Walid Soliman, Salah Mohsen na Hussein El-Shahat kwa sababu tofauti.

Nafasi za nyota hao zinatarajiwa kuzibwa na wachezaji Wahid Mahmoud, Mahmoud Kahlaba, Mohamed Magdy, Mohamed Sherif na Ayman Ashraf..

KOCHA Mkuu wa miamba ya soka Tanzania, Didier ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi