loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

JPM afafanua vita ya corona

RAIS John Magufuli amesema, changamoto za sasa ukiwemo ugonjwa wa COVID-19 unaosababishwa na virusi vya corona ni majaribu na yatapita.

Aliyasema hayo jana alipoungana na waumini wa Parokia ya Mtakatifu Petro, Oysterbay jijini Dar es Salaam kusali Misa Takatifu ya Jumapili (Dominika ya 1 ya Kwaresma).

Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa, ilieleza kuwa, Rais pia aliwashukuru Watanzania kupitia madhehebu ya dini kwa kuitikia mwito wa maombi na kufunga ili Mungu aepushe ugonjwa wa COVID -19.

Alisema, Wakristo waliopo katika kipindi cha Kwaresma na Waislamu ambao wanakaribia kuanza mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, waendelee kumuomba Mungu ili pamoja na jitihada za kibinadamu Mungu ndiye muweza wa yote.

Magufuli alisema huu ni wakati wa kumuomba sana Mungu na pia Watanzania waendelee kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa COVID- 19 kwa kuzingatia maelekezo ya wataalamu wa afya.

Alisisitiza kuwa serikali haijazuia kuvaa barakoa kujikinga kuambukizwa virusi vya corona ila Watanzania wachukue tahadhari kwa kutumia barakoa zinazotengezwa nchini zikiwemo za Bohari ya Dawa (MSD) au wanazozitengeneza wenyewe kwa kuwa kuna mashaka kuhusu usalama wa barakoa zinazoingizwa kutoka nje ya nchi.

Aidha, Rais Magufuli alisisitiza kutumia njia za asili za kukabiliana na magonjwa ya kupumua ukiwemo ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kujifukiza.

Aliwataka Watanzania waondoe hofu kwa kuwa ina madhara zaidi, na akasisitiza waendelee kumtumaini na kumtanguliza Mwenyezi Mungu.

Magufuli alisema kumuomba Mungu ni muhimu kwa kuwa njia za kujikinga kwa barakoa, kutogusana, kutokaribiana na kujifungia majumbani zimeonekana kutokuwa suluhisho la uhakika kwa kuwa mataifa yanayofanya hivyo watu wake wanapoteza maisha kwa maelfu ikilinganishwa na Tanzania.

Alimpongeza Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro, Oysterbay, Padre Dk Alister Makubi kwa mahubiri yaliyoeleza namna Yesu alivyojaribiwa.

JOPO la Majaji 12 nchini Marekani limemtia hatiani ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi