loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Makamu wa Rais afungua mkutano wa uwekezaji sekta ya madini

Makamu wa Rais, Samia Suluhu leo amefungua Mkutano wa  Kimataifa wa Uwekezaji Katika Sekta ya Madini  Tanzania 2021 ambapo amewataka wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali duniani kuja kuwekeza katika sekta hiyo.

Akizungumza katika hotuba yake Jijini Dar es Salaam, Suluhu amebinisha kuwa kwa mwaka jana sekta hiyo ndiyo iliongoza kwa ukuaji kwa 17.7% pamoja na uuzaji wa vito vya thamani kubwa nje ya nchi hivyo kuvutia wawekezaji wengi.

“Niungane na wito wa kiongozi wetu Rais Magufuli kuwakaribisha nchini wale wote mnaofuatilia kongamano hili (kwa njia ya video)  na wengine wenye nia ya kuja kuwekeza katika sekta hii hapa nchini inayokuwa kwa kasi kubwa sana “ amesema Suluhu.

Aidha, Suluhu amesema kuwa pamoja na janga la corona lililokumba dunia kuipa changamoto ya uzalishaji na soko la uhakika  sekta hiyo lakini  mwaka jana Tanzania ilikuwa miongoni mwa nchi tano barani Afrika ambazo ni wazalishaji  wakubwa wa madini ya dhahabu.
-

MAMLAKA ya Mawasiliano (TCRA), imezitaka kampuni za simu ...

foto
Mwandishi: Alfred Lukonge

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi