loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Simba ni jasho  na damu leo

SIMBA imejipanga kuingia na mbinu mpya zitakazo wawezesha kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa pili wa hatua ya makundi wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri utakaopigwa leo kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Timu hizo zinaingia kwenye mchezo huo zikiwa na kumbukumbu yakuanza vyema kwenye mechi zao za kwanza, ambapo Simba ilishinda ugenini bao 1-0 dhidi AS Vital ya Jamhuri ya Kideomkrasia ya Congo (DR), wakati Al Ahly ikishinda nyumbani mabao 3-0 dhidi ya Al Merrikh ya Sudan.

Uzito wa mchezo wa leo unachagizwa na historia iliyoweka Simba ikiwa nyumbani kwa kushinda dhidi ya klabu za Misri, ambapo msimu wa mwaka juzi ilishinda bao 1-0 dhidi ya Al Ahly kwenye mchezo wa hatua kama hiyo.

Al Ahly ambayo iliifunga Simba 5-0 msimu huo katika mechi ya awali, itaingia kwenye mchezo huo ikijivunia mafanikio waliyopata kwani wao ndio mabingwa watetezi na ni washindi wa tatu wa Kombe la Dunia kwa vilabu.

Pamoja na ubora wa Simba yenye rekodi ya kutumia vema uwanja wa nyumbani, Al Ahly sio timu ya kuibeza kwani ina uwezo mkubwa wa kushinda hata ugenini.

Vile vile ina kocha anayetoka Afrika Kusini, Pitsone Mosimane ambaye analijua vizuri soka la Afrika baada ya kuipatua mafanikio Mamelodi Sundowns ya nchini kwao ambayo iliwahi kuiondoa Al Ahly katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kuelekea kwenye mchezo huo, kocha msaidizi wa Simba, Selemani Matola alisema wachezaji wote wako salama na kilichobaki ni jukumu la kocha mkuu wa timu hiyo kuchagua wachezaji watakaoanza kuwakabili Wamisri hao.

Alisema mchezo huo hautakuwa rahisi kwani wapinzani ni timu imara na wanaiheshimu kwa kufanya vizuri katika michuano ya Afrika.

 “Michuano hii ni ya mabingwa, hivyo hakuna timu dhaifu, kikubwa tumejipanga pamoja na kwamba tunakutana na kikosi bora kuhakikisha tunapata ushindi katika mchezo wetu wa nyumbani,” alisema.

Matola aliwaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kuitia moyo timu yao kwani shabiki ni mchezaji wa 12 na wao wanataka kuwafurahisha mashabiki wao.

Naye kocha wa Al Ahly, Mosimane alisema wapo tayari kuwakabili Simba na hawana hofu na muda uliopangwa kuchezwa mchezo huo was aa 10:00 jioni na kwamba hategemei kubadili wachezaji kwa sababu ya hali ya hewa.

“Tupo tayari kwa mchezo na hakuna la kuhofia na muda wa mechi si sababu ya kubadili kikosi tupo tayari kwa mapambano, " alisema Mosimane.

Naye nahodha wa Simba, John Bocco ambaye kwa muda mrefu ni majeruhi alisema wachezaji wa timu hiyo wamejipanga vizuri na wana amini wanaenda kucheza mchezo huo wakiwa na morali kubwa ya kutafuta  ushindi

KOCHA Mkuu wa Coastal ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi